Mama Kikwete kwenye mkutano wa SADC, Maputo-Msumbiji

Mama Salma Kikwete na kulia mke wa rais wa zambia Dr. christine kaseba wakiufurahia azimio la mkataba wa kuondoa ukimwi kati ya mama kwenda kwa mtoto mkataba uliofanyika mjini maputo msumbiji .

Mama Kikwete kwenye mkutano wa SADC, Maputo-Msumbiji

Mama Salma Kikwete na kulia mke wa rais wa zambia Dr. christine kaseba wakiufurahia azimio la mkataba wa kuondoa ukimwi kati ya mama kwenda kwa mtoto mkataba uliofanyika mjini maputo msumbiji .

Mama Kikwete kwenye mkutano wa SADC, Maputo-Msumbiji

Mama Salma Kikwete na kulia mke wa rais wa zambia Dr. christine kaseba wakiufurahia azimio la mkataba wa kuondoa ukimwi kati ya mama kwenda kwa mtoto mkataba uliofanyika mjini maputo msumbiji .

Mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana

Mama Salma Kikwete na kulia mke wa rais wa zambia Dr. christine kaseba wakiufurahia azimio la mkataba wa kuondoa ukimwi kati ya mama kwenda kwa mtoto mkataba uliofanyika mjini maputo msumbiji.

Mpango kasi wa kuwawezesha wanawake na wasichana

Mama Salma Kikwete na kulia mke wa rais wa zambia Dr. christine kaseba wakiufurahia azimio la mkataba wa kuondoa ukimwi kati ya mama kwenda kwa mtoto mkataba uliofanyika mjini maputo msumbiji.

Saturday, September 1, 2012

Wake wa Marais wa SADC wasaini Azimio la kupunguza VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto. Aug 19, 2012


Wake wa viongozi wa wakuu wa nchi na Serikali za Kusini mwa Afrika (SADC) wamepitisha azimio la kutokomeza maambukizi ya Virusi Vya Ugonjwa wa Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kuhakikisha kuwa wanapunguza vifo vya kina mama na watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi.

Azimio hilo lilisainiwa jana mjini Maputo na wake wa wakuu wa nchi za SADC waliohudhuria mkutano wa siku mbili wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni hitaji la awali kwa maendeleo ya Kikanda ulioenda sambamba na mkutano wa 32 wa SADC.

Akisoma Azimio hilo mbele ya waandishi wa habari, Katibu wa kamati iliyoandaa azimio hilo Daud Nasibu alisema kuwa nia kubwa ya SADC ni kuimarisha biashara na mahusiano ya kikanda ambayo matokeo yake ni kusafiri kwa watu na bidhaa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine jambo linapelekea kupatikana kwa ajira na kupunguza umaskini lakini kwa upande mwingine kumekuwa na kasi ya maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ukimwi.

Nasibu alisema kuwa wake hao wa wakuu wa nchi watahakikisha kwamba wanafanya kazi na Serikali za nchi zao pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kupunguza maambakizi ya ugonjwa huo na kutokuwa na maambukizi katika nchi zao kwani wanaamini kuwa inawezekana kwa kizazi kijacho katika SADC kuzaliwa kwa watoto wasiokuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

“Tutawahamasisha wanawake ili waweze kuhudhuria katika vituo vya Afya na kupata huduma za mama na mtoto ikiwa ni pamoja na huduma ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) kabla na baada ya kujifungua.
“Pia tutawahamasisha viongozi wa sekta zote wakiwemo wa dini, wa Serikali na wa jadi pamoja na wakunga wa jadi ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja katika jitihada zetu za za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika nchi za kanda ya Kusini mwa Afrika”, lilisema Azimio hilo.

Kwa upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa kitu kikubwa ni kuhakikisha kwamba azimio walilolisaini likishapata baraka za wakuu wa nchi lianze kufanyiwa kazi ili kuweza kutimiza lengo walilojiwekea la kutokomeza janga la Ukimwi ambalo ni tishio kwao, kwa vizazi vyao na vizazi vijavyo.

“Sisi kama wake wa wakuu wa nchi za SADC ambayo ina nchi wanachama 14 sote tukiwa na sauti moja kwani jambo hili linatuhusu wote, hakuna kitu kitakachoshindikana na tutaweza kupambana na kutokomeza ugonjwa huu ambao unatishia maendeleo ya nchi zetu na Dunia kwa ujumla”, alisema Mama Kikwete.

Naye Rais wa Umoja wa wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi (OAFLA) ambaye pia ni Mke wa Rais wa Namibia Penehupifo Pohamba aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kusema kuwa kazi iliyobaki ni moja ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa malengo waliyojiwekea yanatimia.

Mama Pohamba alisema, “Mimi kama rais wa OAFLA nimefurahi sana kwani hivi sasa nimepata nguvu kwa kuwa tunaazimio ambalo linatubana katika kufanya kazi zetu hivyo basi nitahakikisha kuwa malengo yetu yanafanikiwa, jambo la muhimu ni kwetu sote kufanya kazi kwa pamoja”.

Ugonjwa wa Ukimwi umekuwa ni tishio Ulimwenguni hususani kwa maendeleo ya nchi zinazoendelea kwani takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2011 zaidi ya watu milioni 34 wanamaambukizi ya VVU kati ya hao milioni 30.7 ni watu wazima, milioni 16.7 wanawake na milioni 3.4 watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.

Zaidi ya watoto 1000 wanufaika na ufadhili wa WAMA. July 27, 2012


Zaidi ya watoto wa kike na wa kiumeelfu moja ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa yote nchiniwamenufaika na ufadhili wa masomo unaotolewa naTaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)iliyopo jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo wakati akiongea kwenye mkutano wa saba wa wake wa marais wa Afrika uliozungumzia masuala ya amani barani Afrika uliomalizika leo mjini Abuja nchini Nigeria.

Mama Kikwete alisema kuwa kati ya wanafunzi waliopata ufadhili huo 532 wanasoma elimu ya Sekondari katika shule mbalimbali hapa nchini, 250 wanasoma shule ya Sekondari ya mfano yawasichana inayomilikiwa na Taasisi hiyo yaWAMA-NAKAYAMA iliyopo Rufiji Mkoani Pwani na wanafunzi 12 wanasoma vyuo vya elimu ya juu.

“Taasisi yangu imejenga Shule ya Sekondari ya kata inayomilikiwa na Serikali ya Nyamisati pamoja na nyumba za walimu ambapo jumla ya wanafunzi 320 wanasoma katika shule hiyo, pia tumeweza kujenga mabweni ya wasichana katika shule mbalimbali zasekondari.

Tumechangia elimu kwa kutoa vitabu milioni moja, madawati, vitanda, magodoro na kufunga umeme wa jua kwenye baadhi ya shule zisizokuwa na umeme”, alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA”, alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA.

Kwa upande wa afya, Mama Kikwete alisema kuwa kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) wamekuwa wakitumia kampeni ya mtoto wa mwenzio ni wako mkinge na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ambayo lengolake kuu ni kupunguza maambuikizi ya ugonjwahuo kwa watoto na vijana.

Pia Taasisi hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya afya ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito nawatoto katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali71, kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa mpango wa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT) katika mikoa ya Tabora, Pwani, Kagera, Kigoma na Mtwara.

Mama Kikwete alisema, “Tumeweza kuwasaidia na kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kutoa msaada wa kifedha kwa vikundi 89 vya Benki za maendeleo vijijini (VICOBA) na Vikundi vya kuweka Akiba na Kukopa (SACCOs), kutoa mafunzo ya ukulima wa zao la pilipili aina ya Paprika kwa wakulima 134 na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake 400katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Alimalizia kwa kusema kuwa, Taasisi ya WAMA imeweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa maafisa maendeleo ya jamii katika mikoa ya Lindi ambao waliweza kuvifundisha vikundi vya wanawake katika maeneo ya vijijini, kutoa mafunzo ya Ukimwi na virutubisho vya mwili kwa wanawake 100 na usindikaji wa vyakula kwa wanawake 120 katika mikoa ya Arusha na Pwani.

Taasisi ya WAMA ilianzishwa mwaka 2006 huku ikiwa na malengo ya kumuinua mwanamke kiuchumi, kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanaotoka katika mazingira hatarishi wanapata elimu na kuimarisha afya ya mama wajawazito na watoto.

NHIF yatoa somo kwa wanavikundi walio chini ya WAMA jijini Dar es salaam.June 16, 2012


Jumla ya wanavikundi 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wameridhishwa na utaratibu wa huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hatua iliyowafanya kuahidi kujiunga mara moja ili wawe na uhakika wa kupata matibabu.

Hatua hiyo imefikiwa wakati wa mafunzo yaliyotolewa na NHIF kwa wanavikundi hao Dar es Salaam leo ambapo w alielezwa faida wanazoweza kupata kupitia utaratibu wa kujiunga na Mfuko huo.Kutokana na hatua hiyo, NHIF kwa kushirikiana na WAMA wataandaa utaratibu utakaowawezesha wanavikundi hao kuanza utaratibu huo mara moja ambao utawanufaisha na kuwapunguzia mzigo wa gharama za matibabu.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika sekta ya afya, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuwa na dhamira ya kuwapatia watanzania wote utaratibu unaoeleweka wa huduma za afya na kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma za matibabu kwa heshima inayostahili.

“Utaratibu wa kupata tiba kwa kadi unao manufaa makubwa kwenu, kwani gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa mno na kama mnavyoelewa ugonjwa haupigi hodi hivyo kwa kuwa na kadi itasaidia kupata matibabu wakati wowote hata kama hamtakuwa na fedha kwa muda huo,” alisema Mikongoti.

Mafunzo ya wanavikundi hao ni mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa na Mfuko kwa viongozi wa vikundi ambayo yalikuwa na lengo la kuwapa elimu juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

“Tuko hapa ili tuzungumze fursa na vikwazo vinavyoweza kuukabili mpango wa Bima ya Afya kwa Wajasiriamali,.. dhana hii bado ni ngeni kwa wengi lakini inaweza kuwa na manufaa kwa kuielewa na kuifanyia kazi na sisi kama Mfuko tumejipanga kuhakikisha huduma hii mnaipata kama inavyotakiwa” alisema Mikongoti.

Katika mkutano huo Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Rehani Athumani ambaye aliwasilisha mada iliyohusu huduma za matibabu za uchangiaji kupitia NHIF na CHF ikiwa ni pamoja na manufaa yake.

Rehani aliwaeleza wanavikundi hao kuwa endapo watajiunga na Mfuko huo watapata huduma za matibabu katika hospitali zote za Serikali na za binafsi ambazo zimesajiliwa na Mfuko huo.

Alisema kuwa katika kuhakikisha wanachama wa Bima ya Afya hawakumbani na tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma, Mfuko pia umesajili maduka ya dawa ambayo mwanachama anaweza kupata huduma ya dawa kama atakosa huduma hiyo katika kituo cha matibabu alichokwenda.

Kutokana na hali hiyo, aliwaomba kujiunga na Bima ya Afya ili wanufaike na mtandao mkubwa wa huduma za matibabu.

Hata hivyo Rehani hakusita kuwakumbusha wajibu wa kuwa walinzi wa huduma za afya hasa pale wanapoona kasoro za kiutendaji katika vituo vya huduma za matibabu.

Kwa upande wa wanavikundi hao, waliweka wazi msimamo wao kuwa wako tayari kujiunga na utaratibu wa Bima ya Afya ili waweze kunufaika na matibabu hatua ambayo itawapa uhakika zaidi wa kuendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa kuwa mtaji wa masikini ni afya yake mwenyewe.

Kukubali kwa wanachama hao kujiunga na Bima ya Afya ni moja ya mafanikio makubwa ya WAMA ambayo lengo lake kubwa ni kuhakikisha inawaunganisha wajasiliamali hao na watoa huduma kama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

WAMA Foundation Women Groups Empowered on Access to Health Insurance Services, May 26, 2012 - Dar es Salaam


WAMA Foundation in collaboration with National Health Insurance Funds of Tanzania (NHIF) has conducted a one day workshop to the 52 leaders of WAMA Foundation Women Groups at Majohe, Pugu known as Umoja wa Vikundi vya WAMA kata ya Majohe (UVIMA) and their neighbor groups at Mbagala, Mwisho wa Lami and Pugu.

The workshop was conducted at WAMA Foundation ground on May 26, 2012. It was facilitated by the team from National Health Insurance Fund (NHIF) and WAMA Foundation: Mrs. Tabu Likoko, Director of WAMA Women Economic Empowerment Unit, Eugene Mikongoti, Director of Operations of NHIF, Mr. Rehani Athumani, Acting Director Community Health Fund (CHF), Mr. Michael Mhando, Director of Health Insurance Services, NHIF, Mrs. Grace Michael, Public Education and Relations Officer, NHIF and Ms. Philomena Marijani, Advocacy and Communication Officer- WAMA Foundation.

The workshop aimed at educating the Women Groups on available services and benefits of National Health Insurance services so as they can be members of the fund and improve their well being. The presentations discussed on the available packages and benefits of National Health Insurance Fund schemes namely The Health Insurance Fund (NHIF), Community Health Fund (CHF) and the introduction of private and informal sector beneficiaries’ member.

After the presentations and discussions the participants decided that they will join the National Health Insurance Fund (NHIF) of which has many benefits compared to Community Health Fund (CHF).

Giving the final remarks, Director of Women Empowerment Unit, Mrs. Tabu Likoko encouraged the women to work hard and to be proactive and punctual on all their activities. She told them that as the leaders they had a major role of educating other on the knowledge they have got on National health Insurance Service so as they can bring a change in their society especially in increasing access to better health for all citizen.

As the National Health Insurance Fund indicated that the total of 6.2 million people from formal and non- formal sectors are beneficiaries of NHIF and CHF. WAMA Foundation sees the importance of linking the women groups with National Health Insurance Fund so as they can benefit from their service especially on acquiring better health services.

Mama Kikwete ahimiza ushirikiano na NGOs za Marekani kuinua Afya ya mtoto na mama. May 19, 2012

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahimiza wadau afya na lishe kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na taasisi za Kitanzania na Serikali kwa ujumla ili kuinua afya ya mtoto na mama nchini Tanzania.

Aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa pamoja na NGO sita za kimarekani zinazofanya kazi mbalimbali nchini Tanzania kwenye masuala ya lishe na afya tarehe 18 Mei 2012. Taasisi zilizohudhuria mkutano huo ni Malaria No More, Health Overseas Volunteers, Path International, Save the Children, Global Health and Diplomacy na Africare International, uliofanyika pembezoni na mikutano ya Rais Kikwete kuhusu masuala ya usalama wa chakula na lishe duniani.

Katika hotuba yake na taasisi hizo, Mama Salma Kikwete alizishukuru taasisi hizo kwa kufanya kazi Tanzania ili kusaidia taifa kufikia malengo yaliyowekwa kwenye dira ya taifa kuhusu masuala ya afya. Alihimiza ushirikiano na taasisi nyingine za Kitanzania hususan kwenye masuala ya uhamashaji, utoaji wa elimu na kujenga uwezo kwa Watanzania kwenye masuala ya lishe.

Akijibu swali la mtaalamu wa usalama wa chakula na lishe kutoka USAID Bi. Laura Birx, Mama Salma Kikwete alisema msaada mkubwa unaohitajika kwa Watanzania ni rasilimali fedha na elimu ili kuinua hali ya lishe kwa watoto wa Tanzania.

“Kwenye maeneo mengi mijini, elimu kuhusu lishe ni muhimu zaidi kwani baadhi ya familia wanauwezo wa kifedha na wanachohitaji sana ni elimu kuhusu lishe” Alisema Mama Kikwete.

Hii inatokana na hali ya maisha ya mjini ambapo wazazi wengi wanajikita na kazi na kuacha walezi wa nyumba kufuatilia lishe ya watoto. Alisema elimu kwa walezi hao ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwa watoto hao wanapewa lishe bora.

Hivi karibuni USAID kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali imetoa fedha $ 30 milioni kutekeleza mpango wa lishe Tanzania. Mpango huo ujulikanao kama Mwanzo Bora Nutrition Program unatekelezwa kwenye mikoa mitatu ya Manyara, Morogoro na Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano. Mpango huo utakapokamilika utasaidia Serikali kujenga uwezo wa kutoa elimu kuhusu lishe, kuinua hali ya lishe ya watoto wadogo, wakina mama wajawazito na wanaonyonyesha.

Mkutano wa Mama Salma Kikwete na taasisi hizo ulioratibiwa na Africare kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Marekani, umefungua milango ya ushirikiano baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na taasisi hizo sita ili kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu umuhimu wa afya bora na lishe kwa watoto.

Kwenye ziara hiyo, Mama Kikwete na ujumbe wake pia walitembelea Hospitali Kuu ya Watoto Washington DC ya Children’s National Medical Center na kutembelea wodi ya watoto wenye mahitaji maalum. Wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Hospitali hiyo kwenye masuala ya Uhusiano ya Kimataifa Dkt Jerome Paulson alikubaliana na Dkt Hadija Hemedi Mwamtemi, Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuanza mazungumzo ya kushirikiana kwenye kuelimisha walimu (Training of trainers) watakaofundishwa wengine kuhusu afya ya msingi kwa watoto ili kujikinga na magonjwa yatokanayo na uharibifu wa mazingira.

Dkt. Paulson alisema mpango huo wa kutoa elimu kwa watoa huduma ya afya kwa watoto hauna gharama kubwa lakini matunda yake yataonekana kwa kuwa na watoto wenye afya bora baada ya kuwalinda na magonjwa kama vile pumu yatokanayo na uchafuzi wa hewa.

Kwa upande wake Mama Salma Kikwete aliwasihi washirikiane na Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kwa pamoja kuanzisha mpango huo wa kubadilishana uzoefu na kupeana ujuzi (TOT) ili kulinda afya ya watoto wa Tanzania.

Mama Salma Kikwete alifanya ziara hiyo wakati Rais Kikwete akihudhuria Mkutano wa mwaka kuhusu Kilimo na Usalama wa Chakula Duniani Washington DC, Marekani.